Shirika la Habari la Hawza - Imamu Sajjad (sa) anamwomba Mwenyezi Mungu kwa kutumia maneno haya:
«اللَّهُمَّ ... اسْتَعْمِلْنِی بِمَا تَسْأَلُنِی غَداً عَنْهُ.»
Ee Mwenyezi Mungu! Nitumikishe mimi katika mambo ambayo kesho Siku ya Kiyama utanihesabia kwayo. (1)
Sherehe:
Dua kama hii pia imepokewa kutoka kwa Bibi Fatima Zahra (sa) na Imamu Sadiq (as).
Dua hii inaweza kuwa kama taa ya mwongozo inayomsindikiza mwanadamu daima — hasa vijana na barobaro wenye shauku ya dini ambao wapo katika mwanzo wa safari ya kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mwanadamu katika maisha yake anakabiliana na njia na chaguo nyingi, lakini swali muhimu n hilii: ni njia ipi kati ya hizo inayoweza kumsaidia zaidi na vizuri zaidi kwene njia ya uchaji na utiifu kwa Mwenyezi Mungu?
Kupitia dua hii, kwa hakika tunamwomba Mwenyezi Mungu hivi: Ee Mola! Weka mapenzi yangu, kipawa changu, uwezo wangu na fursa zilizoko mbele yangu zote katika njia inayokupendeza Wewe; na zitumie kwa ajili ya utiifu kwako.
Na bila shaka, ili kufikia lengo hili, ni lazima mtu ajitoe kwa uwezo wake wote. Ndiyo maana Imamu wa wachamungu (as) alimwomba Mwenyezi Mungu kwa maneno haya:
«یَا رَبِّ یَا رَبِّ یَا رَبِّ، قَوِّ عَلی خِدْمَتِکَ جَوارِحِی، وَاشْدُدْ عَلَی الْعَزِیمَةِ جَوانِحِی.»
Ee Mola wangu, Ee Mola wangu, Ee Mola wangu! Viimarishe viungo vyangu kwa ajili ya kukuhudumia, na uitie nguvu azma ya moyo wangu. (2)
Ikiwa tutatafuta tafsiri ya kisasa ya maneno haya ya Amirul-Mu’minin (as), tunaweza kusema: “Ee Mola! ‘Nyenzo ngumu’ na ‘nyenzo nyepesi’ zilizopo kwangu mimi zitumie kwenye njia ya kukuabudu wewe.”
Na huenda maneno yanayoweza kukusanya maana ya dua hizi zote yakapatikana katika kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliposema:
«اَللَّهُمَّ لاَ تَکِلْنِی إِلَی نَفْسِی طَرْفَةَ عَیْنٍ أَبَداً.»
Ee Mwenyezi Mungu! Usiiachie nafsi yangu hata kwa muda wa kufumba na kufumbua macho. (3)
Rejea:
1. Sahifa Sajjadiyya, Dua ya 20 (Dua ya Makarim al-Akhlaq).
2. Dua ya Kumayl.
3. Al-Manaqib, Juzuu ya 1, uk. 57.
Imeandaliwa na Kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza.
Maoni yako